NTSA yapata pigo lingine baada ya mahakama kutoa uamuzi huu
- NTSA imepata pigo lingine tena baada ya mahakama kutangaza kuwa kupigwa marufuku kwa safari za usiku kwa magari ya umma sio halali
- Akitoa uamuzi wake dhidi ya madereva 13 waliokamatwa kwa kusafirisha abiria usiku,hakimu mkuu wa mahakama ya Nakuru alisema kuwa hakuna sheria inayopinga safari za usiku
- Shirika hilo lilikuwa limepiga marufuku safari za usiku kama njia moja ya kupunguza ajali za barabarani
- Aidha,Rais Uhuru Kenyatta aliwaamuru maafisa wa NTSA kuondoka kwenye barabara na kuachia maafisa wa polisi wa trafiki kazi ya kulinda usalama barabarani
Shirika la usalama barabarani,NTSA limepata pigo kubwa baada ya mahakama kuamuru kuwa hakuna sheria inayopinga safari za usiku kwa magari ya umma.
Habari Nyingine: Kuingia Mombasa rahisi, kutoka matanga-hii ndiyo sababu
Akitoa uamuzi wake dhidi ya madereva 13 waliokuwa wamekamatwa kwa kuendesha magari ya umma usiku, hakimu mkuu wa mahakama ya Nakuru alisema kuwa amri hiyo ya NTSA haikuwa halali.
Kulingana na jaji Nancy Makau, madereva hao hawakuwa na hatia yoyote ya kutiwa mbaroni.
Uamuzi huo unatokea siku chache tu baada ya rais Uhuru Kenyatta kuamrisha kuondolewa kwa maafisa wa NTSA kwenye barabara kufuatia kero la ongezeko la ajali katika sehemu kadhaa za nchi.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Habari Nyingine: Naibu gavana wa Nairobi, Polycarp Igathe ajiuzulu - adai kuhangaishwa na Sonko
Shirika la NTSA lilikuwa limepiga marufuku usafiri wa magari ya umma usiku likidai kuwa ni njia moja ya kupunguza ajali za barabarani.
Utafiti wa hivi majuzi unaonyesha kwamba zaidi ya watu 400 wamepoteza maisha yao kwenye ajali za barabarani hasa msimu wa krismasi.
Habari Nyingine: Cristiano Ronaldo ‘aliiba’ tuzo langu la Ballon d'Or-nyota wa Bayern Munich adai
Sasa baadhi wa Wakenya na wanasiasa wanataka shirika hilo kufutiliwa mbali kwa sababu limeshindwa kutekeleza wajibu wake.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una taarifa ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4BxfY9mpa2rkWLGorzArZhmqJmcvG64yKeeoqaVYq%2BircOaZLKZXaKuqa3KmqSaZZuqwbCtjK6Ypq2qnnqpwdRnn62lnA%3D%3D