Mike Sonko amfuta kazi meneja wa idara ya kupigana na moto kwa kufeli kikazi
- Gavana Mike Sonko wa Nairobi amempa likizo ya lazima kufuatia mkasa wa moto uliowaua watu wanne katika eneo la Lang'ata
- Katika barua iliyoonekana na TUKO.co.ke, Sonko alimshtumu afisa huyo kwa kukosa kufanya kazi ya kama inavyohitajika
Gavana wa kaunti ya Nairobi, Mike Sonko mnamo siku ya Jumatatu, Januari 29 2018 alimfuta kazi afisa anayesimamia idara ya kupambana na mikasa ya moto jijini Nairobi, Brian Kisali, kwa kukosa kuwajibika katika kazi yake.
Habari Nyingine: Je wanaume wanahitaji nini katika uhusiano? Wakenya watoa maoni yao
Hii ni baada ya kuzuka kwa moto katika eneo la Lang'ata uliowaua watu wanne.
Sonko alimpa Kisali barua rasmi ya likizo ya lazima, msingi mkuu ikiwa ni visa vingi vya kuzuka kwa moto vinavyoshuhudiwa mara kwa mara.

Habari Nyingine: Mambo 14 ya uongo ambayo wazazi huwaambia watoto wao
Kulingana na mkuu wa utumishi katika kaunti hiyo, Leboo Ole Morintat, afisa huyo alikosa kutekeleza majukumu makuu ya kikazi aliyopewa.
"Ulifahamu kuwa moto huo ulizuka katika eneo la Langata South Land tarehe 28 Januari 2018 jioni na timu yako ikakosa kuwasiliana vizuri na kusababisha maafa na uharibifu wa mali nyingi...Unaagizwa kuendelea na likizo ya lazima haraka iwezekanavyo...hadi pale utakapoitwa," Alivyoandikiwa katika barua.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Habari Nyingine: Dada wawili mapacha wafanya harusi ya kifahari Lagos (picha)
William Ruto alisafiri kuelekea eneo la mkasa huo na kuwafariji waliofiwa na kupoeteza mali zao.
Kama ilivyoripotiwa na TUKO.co.ke, moto huo ulizuka katika mtaa wa mabanda Lang'ata na kudumu kwa muda mrefu bila hata zima moto wa kaunti kuingilia kati hata kuwasili.

Ilisemekana kuwa lori za kaunti zilifika hapo na hazikuwa na maji.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4F2fpZmpKKjlWLAsLrKqGSapZaqwaJ5ypqxomWdmrumtsBmrpplmZmus62Msphmo6WltqitzZpkp5ldory1u4ykrpplm6qzprjIZqKio5Gvtm%2B006aj